Wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi ZAMZAM mjini BUKOBA wakivua samaki katika mto wenye maji machafu wa KANONI karibu kabisa na ofisi za Manispaa, muda wa saa tano asubuhi ambapo walitakiwa kuwa darasani.
Ni jambo la kusikitisha kuona wazazi na walezi wakiwakuta watu hawa katika mazingira yanamna hiyo lakini hakuna anayekemea jambo hilo, je walimu hawajiulizi kwamba wanafunzi hawa wako wapi katika muda wa kuwa darasani?
Huyu siyo kwamba amepumzika, ni mtu ambaye kafa baada ya kipigo kutoka kwa raia kwa mujibu wa vyanzo vyetu. Jamaa aliyefahamika kwa jina moja tu la NURU na inasemekana alikuwa akiishi katika vichaka vya NYAKANYASI mjini Bukoba, amekutwa amekufa karibu kabisa na daraja linalotenganisha mtaa wa nyakanyasi na USWAHILINI mjini Bukoba.
Miongoni mwa waliskia purkushani za usiku wakti wananchi wakitoa kichapo, wanasema waliskia sauti zikisema kama ndizi lakini hawakujua kulichoendelea.
Pembeni ni mizigo ya nguo inayosadikiwa kuwa ni ya wizi. Kumekuwa na matukio ya mauaji mjini bukoba ambapo m,apema mwezi uliopita mwanamke mmoja aliyefahmika kwa jina moja la NYANGOMA alikutwa amekufa katika mtaa wa BUYEKERA kata BAKOBA mjini BUKOBA wakti huo akiwa amevuliwa nguo yake ya ndani (chupi) na imetupwa pembeni